Miaka 5–12

Kadogoo Club
Watoto wakisoma kitabu cha Kadogoo Mtalii

Kadogoo Club

Sisi ni Washindi!

Jumuiya ya watoto wenye umri wa miaka 5–12 — kujifunza, kusoma, kucheza na kuifahamu Tanzania.

Anza safari

Jiunge na Kadogoo Club

Jaza taarifa za mtoto na mzazi au mlezi — uanze kujifunza, kusoma na kushinda pamoja.

  • Watoto wenye umri wa miaka 5–12
  • Vitabu, matukio na mashindano
  • Jamii inayojenga washindi

Jiunge na Kadogoo Club

Anza hapa — utakamilisha fomu kamili

Taarifa zako zitahifadhiwa kwenye fomu kamili.

Vitabu

Vitabu vya Kadogoo Mtalii

Mfululizo wa vitabu — kila nakala ina QR code ya kipekee.

Kadogoo Mtalii #2: Kadogoo Mtalii #2 — Hifadhi ya Tarangire#2

Kadogoo Mtalii

Kadogoo Mtalii #2 — Hifadhi ya Tarangire

Tarangire

Agiza nakala →
Kadogoo Mtalii #3: Kadogoo Mtalii #3 — Kisiwa cha Zanzibar#3

Kadogoo Mtalii

Kadogoo Mtalii #3 — Kisiwa cha Zanzibar

Zanzibar

Agiza nakala →

Programu

Kile mtoto wako anapata

Vitabu, matukio, mashindano na jamii — yote katika safari moja ya ushindi.

Kadogoo Club

Jumuiya ya watoto 5–12 kujifunza, kucheza na kubuni.

Jiunge zaidi →

Habari

Habari na Matangazo

Habari mpya kutoka Kadogoo Club.

Karibu Kadogoo Club

Announcement

Karibu Kadogoo Club

Jumuiya ya watoto 5–12 — kujifunza, kusoma, kucheza na kushinda.

Vitabu vya Kadogoo Mtalii

Books

Vitabu vya Kadogoo Mtalii

Mfululizo wa vitabu vitano — kila nakala ina QR code ya kipekee.

Kadogoo Road Show
Kadogoo Club road show booth

Bajaji ya Kadogoo inafika shuleni na jamii — Jifunze · Okoa · Cheza · Shinda.

Tazama ratiba →
Kadogoo Festival
Kadogoo Club book launch

Sikukuu ya watoto, vipaji na ushindi — sisi ni washindi!

#1 Kadogoo Mtalii #1 — Kisiwa cha Saanane#2 Kadogoo Mtalii #2 — Hifadhi ya Tarangire#3 Kadogoo Mtalii #3 — Kisiwa cha Zanzibar
Jiunge na Festival
Best reading video

This month’s contest · September

Vote in Community. Winners receive Kadogoo gifts and new books.

Inaisha baada ya siku 1

Kuimba
Kucheza
Kusoma
Kuchora
Hadithi

Nipate Habari Mpya

Watoto wa Kadogoo Club

Kuhusu Sisi

Kadogoo ni Nani?

Kadogoo ni rafiki wa watoto wa Tanzania — anawaongoza kusoma, kubuni, kucheza na kuheshimu mizizi yetu. Kupitia rangi za furaha, maarifa, ndoto, asili na urithi.

Kadogoo Club

Umri 5–12 · Elimu · Ubunifu · Urafiki · Mazingira

Andikisha mtoto

Sheria

Masharti na Sera ya Faragha

Muhtasari wa masharti ya uanachama wa Kadogoo Club.

  1. Kadogoo Club ni kwa watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 12.
  2. Usajili wa mtoto lazima ufanywe na mzazi au mlezi mwenye mamlaka ya kumwakilisha.
  3. Mzazi au mlezi anathibitisha kuwa taarifa zilizotolewa kwenye fomu hii ni sahihi.
  4. Shughuli za Kadogoo Club zinajengwa katika elimu, ubunifu, ushirikiano, heshima, urafiki, utalii na utunzaji wa mazingira.
  5. Mwanachama hataruhusiwa kutumia lugha ya matusi, ubaguzi, vitisho, udhalilishaji au tabia inayoweza kuhatarisha wengine.
  6. Mawasiliano rasmi yanayomhusu mtoto yatafanywa kupitia mzazi au mlezi.
  7. Taarifa binafsi za mtoto hazitachapishwa hadharani. Hizi ni pamoja na namba ya simu, anuani ya nyumbani na taarifa binafsi za shule.
  8. Baadhi ya safari, matukio au mashindano yanaweza kuhitaji ruhusa nyingine ya mzazi na masharti maalumu ya usalama.
  9. Ridhaa ya matumizi ya picha, video na kazi za mtoto ni ya hiari. Mzazi anaweza kuiondoa kwa kuwasiliana na Kadogoo Club.
  10. Kazi ya ubunifu itaendelea kuwa mali ya mtoto. Ruhusa ya kuionyesha haimaanishi Kadogoo Club imepewa umiliki wa kudumu wa kazi hiyo.
  11. Zawadi zitatolewa kwa kuzingatia kanuni za shindano husika. Uanachama pekee hauhakikishi ushindi au zawadi.
  12. Kadogoo Club inaweza kusimamisha uanachama endapo masharti yatakiukwa, baada ya kuwasiliana na mzazi au mlezi.
  13. Mzazi anaweza kuomba taarifa zisahihishwe, mawasiliano yasimamishwe au uanachama wa mtoto ufutwe.
  14. Kadogoo Club itatumia taarifa kwa madhumuni ya uanachama, usalama, uendeshaji wa shughuli na mawasiliano yaliyoidhinishwa.
  15. Kadogoo Club haitauza taarifa binafsi za mtoto au mzazi kwa mtu mwingine.

Washirika

Washirika Wetu

Tunashukuru mashirika yanayotuunga mkono kuwajengea watoto wa Tanzania.